No. 128: Taamini Nitii Pia

Namwandama Bwana kwa alilonena, Njiazangu uning’azia; Na nikimridhisha atanidumisha, Taamini nitii pia.

CHORUS

Kuamini, Njia pweke ni hii Ya furaha kwa Yesu: Amini ukatii.

Giza sina kwangu wala hata wingu, Yeye mara huviondoa; Oga, wasiwasi sononeko, basi; Huamini nitii pia.

Masumbuko yote, sikitiko lote; Kwa mapenzi hunilipia; Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki. Taamini nitii pia.

Mimi sitajua raha sawasawaIla yote Yesu kumtoa; Napata fadhili na radhi kamili, Taamini nitii pia.

Nitamfurahia na kumtumaini, Majumbani na njia-njia; Agizo natenda; nikitumwa hwenda, Huamini nitii pia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *