No. 129: Kumtegemea Mwokozi

Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa; Kukubali neno lake, nina raha moyoni.

CHORUS

Yesu, Yesu namwamini, nimemwona thabiti; Yesu, Yesu yu thamani, ahadi zake kweli.

Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa; Kuamini damu yake nimeoshwa kamili.

Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa; Kwake daima napata, uzima na amani.

Nafurahi kwa sababu nimekutegemea; Yesu, M-pendwa, Rafiki, uwe nami dawamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *