No. 131: Baba Anilinda

Namtegemea Mungu niwapo Humo barani na baharini, Yeye wa mbinguni anilinda. Baba wa mbinguni anilinda.

CHORUS

Namwamini, Mungu anitunza (anitunza) Milimani (milimani) au baharini (baharini), bahariniMoyo wangu (moyo wangu) aulinda (aulinda), Baba wa mbinguni anilinda.

La Waridi alinawirisha, Na huyo tai juu angani, Nami kweli anilinda, Baba wa mbinguni anilinda.

Tunduni mwa simba namwamini,Kwenye vita ama gerezani,Motoni na furikoni, Baba wa mbinguni anilinda.

Bondeni mwa giza na upweke, Mehunga wangu yuanilinda, Kwa upole aniongoza. Baba wa mbinguni anilinda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *