No. 131a: Kwa Mahitaji Ya Kesho

Kwa mahitaji ya kesho, Sina ombi; Unilinde nisitende Dhambi leo; Nisiseme neno baya, Mkombozi, Nisifikiri uovu, Leo hivi.

Ningefanya kazi sawa Na kuomba; Ningekuwa mtu mwema Kila saa; Mapenzi yako nifanye, Na kutii; Nitoe mwili dhabihu, Leo hivi.

Kama leo ningekufa kwa ghafula, Nitegemee ahadi zako Bwana. Kwa mahitaji ya kesho Sina ombi; Uniongoze, nishike Leo hivi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *