Choo, Lavatory

Umewahi ingia katika choo? Kama ndivyo, hata uwe nani wa nani au wa wapi, WEWE NI WETU. Waswahili wengi hupunguza uzito wa maana ya chumba hiki kwa kukiita chumba cha kujisaidia. Choo ni jumba cha maana sana ambacho kila mtu anakihitaji maishani mwake. Kila boma linahitajika liwe na choo. Nilichogundua ni kuwa, wale waume, wazee wa boma wasioweza kutengeneza vyoo kwa mikono yao wenyewe, ni vigumu waenende katika njia za Mungu muumbaji hata waukatae huu ukweli mtupu.

Mijini kuna magari ya kuzoa uchafu wa choo, Exhausters – ‘honey suckers’ yaliyo na maandishi kama ‘wewe ni wetu!’ ‘Yani choo pia ni biashara’ nk. Nikiwa chuoni, kama ilivyo kawaida ya mwanachuo yeyote nilivitumia vyoo vya chuoni.Hivyo vyoo vilikuwa na maandishi yaliyonichekesha sana nilipoyasoma. Wachoraji wa hayo maandishi walikuwa stadi sana katika shughuli yao hivi kwamba hayo maandishi ungeyaona tu pindi ‘ulipoji-set kwa position na kuanza ku-deposit stuff fulani’.

Maandishi yaitwayo toilet literature ‘toilet grafiti.’ Though we want clean lives, we cannot avoid dirt just as we cannot keep flies from mansions nikinukuu baadhi tu, kulikuwa na:

1.“Umeshika nini hiyo mkononi”

2. “If you are doing the right thing, why are you hiding?”

3.“You go to bed with an itching anus; you wake up with a smelling finger!”

4. “Do you write on walls? Tick where appropriate: yes__ No__”

Kulikuwa na mengine mengi yaliyonisukuma kukifinya kicheko chooni kando na shughuli ya uhai iliyonipeleka humo.

Kuna mtu mmoja aliyekuwa ameandika hivi,”Kuhara ni tamu.” Utanisamehe kwa kutumia maneno halisi, lakini ukumbuke si vyema kupunguza maana ya maneno. Badala ya prostitution ama adultery ati tuseme ‘love affair’ si huko kutakuwa kujidanganya. Je huo si upumbavu! Ati tuseme mpango wa kando, NO! sema UMALAYA, UASHERATI! Walioyaandika hayo yote chooni, wote ni wenye akili.

Kuna watu ambao huwa na maringo sana duniani, wajigambao juu ya uwezo wao. Waache wajigambe. Kuna baadhi ya wengine ambao mavazi yao ndiyo nguzo yao. wanaoyajali sana mavazi na mali . Akiwa amevalia nguo fulani ama ana kitu fulani, atawaona wengine kuwa bure, hao pia waachie tu mda kidogo, watapata cha kuwafanya walie, hata kama watalilia chooni.

Mtu akiweza kukudharau jiulize hili swali, “Je, huyu huwa anaenda choo?” Aendaye choo hutoa uvundo, na hata awe kiongozi wa dunia nzima, akinyimwa choo, atajikosea.

Wote tu wahitaji wa choo, na wote ni wahitaji wa MUNGU MUUMBA WETU ambaye alituumba na kutuwekea kiungo cha kwenda choo.Next time ukienda choo shukuru Mungu sana.Kumbuka kuwa ni ujinga kutoenda kanisani siku ya sabato. Ezekiel 20: 12-24.

Asiyeenda kanisani ni sawa na aliye na haja kubwa na hatambui aende wapi. Atasumbuka maishani tena sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *