Ibada inayokubalika na Mungu sehemu ya pili

Ibada inayokubalika Mungu na Mungu ni ibada ya kujitolea kwa hiari. Kisa Katika Biblia ambapo Yesu alikuwa kanisani na waliokuja kanisani walikuwa wakitoa sadaka. Tajiri akatoa pesa nyingi ambapo nia yake ilkuwa ajulikane kwa ukarimu wake kuwa yeye ndiye aliyelisaidia kanisa la Mungu, naye mama maskini akatoa vipande vya fedha viwili tu akiomba moyoni mwake kuwa Mungu ayatende Mapenzi yake kupitia kwa hizo fedha chache. Mungu akasema kuwa yule aliyetoa chache mbele ya watu ametoa nyingi sana. Na yule aliyetoa nyingi mbele ya watu hakuwa ametoa kwa ajili ya upendo kwa Mungu, LA, alitoa ili ajionyeshe, ajulikane.

Ni watu wangapi ambao wamewaua wana wa Mungu ili wapate fedha kwa kumwabudu mfalme wa dunia hii na baada kuzipata wakajivalia nguo za kondoo tukawaona Kwa children’s Homes na mahali pengine pafahamikapo kuwa kuna mahitaji, wakijionyesha ya kuwa wamepeleka msaada, as if wao ndio waletao mvua na kuipa nguvu mimea imee ili iwalishe mabilioni ya watu na wanyama na wadudu na ndege na samaki walio duniani?

Kuna hii issue ya kuanzisha makanisa kila kuchao. Kuna majina Mengi ya makanisa duniani. Na mengi huudhuria ibada zao siku ya jumapili kinyume na mapenzi ya Mungu ambaye anatutaka tushiriki baraka naye katika Sabato.

Wengi wa waumuni wa jumapili ambayo ni siku ya kwanza ya juma, hupamba ibada yao na nyimbo ziletazo msisimko fulani wa kujiona kama wamekaribia moyo wa Mungu. Wengine huomba wakilia na kutubu kwa sauti mithili ya manabii wa Baali walipokuwa wakiomba moto ushuke uteketeze dhabihu yao katika mlima wa Karmeli, Soma 1 Kings 18:19-46.

Manabii wa Baali walijitesa bure! Vilio vyao na kujikata na mayowe na nyimbo zote hazikuwasaidia kitu. Moto haukutokea. Kwa maneno machache tu ya Mtumishi wa Mungu MKUU, nabii aliyeitwa Eliya, Moto ulishuka kutoka mbinguni ukateketeza kafara aliyokuwa ameitoa na baadaye mvua ikanyesha. Kunao wenzio wapendao sarakasi na ngoma. wakizichapa ngoma, akili zao huzuzuliwa, wengine hutumia vileo na mihadarati ikiwamo bangi ili iwazuzue zaidi. Ibada kama hizi ni ibada za hisia, hizi ni ibada za sanamu. Kuna ndugu mmoja aliyekiri kuwa aliupata wendawazimu kwa sababu alikuwa kwa praise and worship team na angehitaji kuzuzuliwa na mihadarati ili awe high. Alichapwa kiboko na Mungu Mwenyewe.

Mungu anapendezwa tunapotii kila atuagizalo. Je, Sauli, Mfalme wa kwanza wa Israeli hakuwa mtume wa Mungu? Na je, alipofikiria kuwa Mungu angependezwa na sadaka za wanyama wanono wanono, si alishindwa KUTII amri ya Mungu ya kuangamiza taifa ovu la Waamaleki. (Soma 1 samwel 15:10-) Alipokataa KUTII amri ya Mungu hata maombi yake na sadaka Zake alizozitoa baadaye akidhani angemuhonga Mungu, vilikataliwa. Kabla aende vitani, Saulo alijiona kuwa angemwomba Mungu tu halafu atimize tamaa zake, hakufaulu kushinda vitani, hakuwa na subira kwa Mungu, aliangamia pamoja na watoto wake akiwamo Jonathan.

So, kama umejua kweli ambayo Mungu anaitaka, ifwate. Ifinyie tamaa yako chini. Tamaa ya mwili inaleta mabishano dhidi ya ukweli wa Mungu.Mungu alitoa Amri kumi za maadili ambazo inampasa kila mwanadamu kuzifwata. Mungu mwenyewe ameahidi kutupa sisi wanadamu uwezo wa kuzishika amri hizo. Amri ya ya nne inaongelea ibada, Soma Exodus 20:8-

Ibada ya Yesu Kristo ambaye sisi ni wafwasi wake, yapaswa kuigwa. Katika ibada zake alikuwa mtulivu. Visa vyake vilikuwa kama hadithi. vilitolewa kwa upole. Kanisa la Mungu lilianzisha pale Eden baada ya Uumbaji, Kanisa liadimishalo uumbaji siku ya Sabato. Siku ya Sabato ni siku ya Jumamosi. Shetani anaipiga vita sabato ya Bwana ndio maana amewainua manabii na mabishops, na waombaji watendao miujiza kwa nguvu za giza ili kupotosha wengi wasioenenda na akili kama Mke wa Loti.

Wengi wa wale wanaoyajaza hayo madhehebu ya siku ya kwanza ya juma badala ya siku ya Sabato wameufwata mfano wa Mke wa Ayubu wa Kumshauri mumewe amtusi Mungu. Wanamtusi Mungu kwa kusema siku ni siku tu. Hapo nyuma kuna wengine niliowasikia wakisema kuwa wanasabato ni waabudu siku, hiyo allegation ni ya ukweli especially kwa watu wajiitao wanasabato ila mienendo yao si ya wanasabato. Hao ndio wale utawaona kwa high-tables wakati wa mlo kanisani, ambao hujitenga na maskini wakala vinono na Ma-pastors. Pata Mengi kama haya kwenye makala ya issues church.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *