Ibada inayokubalika sehemu ya kwanza

Ukisikia neno ibada inayokubalika na Mungu, dhana iibukayo ni kuwa kuna ibada ambayo haikubaliki na Mungu.Lakini kwanza hebu turejelee neno ibada. Neno ibada linaposikika, akili ya mtu hukumbuka kusanyiko la kanisani. Kuna sababu nyingi za kutufanya tukusanyike katika ibada.

Kwanza, Tuingiapo katika ibada huwa tunaashiria utiifu wetu kwa amri ya Mungu aliyoitimiza mwenyewe na kutuamuru sisi pia tukutane. Ukweli mtupu uliopo ni kuwa kama kwako wewe kwenda kanisani siku ya ibada ni jambo gumu, basi huwa hutaki kushirikiana na Mungu Muumba wako.

Ameahidi Mungu Mwenyewe Katika kitabu cha Isaya 58:13 kuwa yeyote ambaye ataacha kufanya mambo yake mwenyewe katika siku ya Sabato , na kuacha idle talk, basi Mungu atamwinua sana katika maisha. Jisomee mwenyewe hilo fungu.

Ibada inaleta amani, ibada ni ya kuleta baraka, katika ibada twafunzwa uumbaji wa Mungu. katika ibada twajua kuwa dhambi ni mbaya, pia twaujua upendo wa Mungu. La muhimu ni tumaini la kuishi milele.

Kuna watu wapumbavu ambao kwa kiburi chao hudhani kuwa huenda kuisoma biblia kanisani kama wasomavyo magazeti au vitabu vya kawaida. Hawa wapumbavu ndio utawakuta wakijigamba-bragging-kuwa wameisoma Biblia mara kadha, From cover to cover. Wale wajuaji wajua kila kitu. Shetani huwaongezea vishawishi vya kubishana didhi ya wale waenezao upendo wa Mungu ili kuwafanya watumishi wa Mungu wafe moyo. Kama wewe ni mmoja wao, ni wakati wako wa kutubu.Mungu amekuwa akikutazama na hata sasa yu macho. Amekuona sasa hivi unaposoma haya mausia. Chunga upumbavu wako usikuletee laana ya milele.

Katika Biblia, kwenye kitabu cha Mithali, wasia umetolewa kwa watu wapigao makelele bila akili kama mikebe kuwa, “Mpumbavu huonekana kama mwenye hekima akiwa mtulivu.” Vyombo vya habari vimekuwa vingi na wapumbavu wamejaa humo nao ndio wamechangia jamii kupoteza maadili, Kelele zao ni kama kelele za wabeba mikongojo kwa mihadhara. Mtu mmoja anaweza kanusha kuwa vyombo vya habari havina madhara lakini ukitaka kuuthibitisha ukweli huu mtupu, waulizeni watoto viumbe alivyoviumba vya kuishi majini. Nakuhakishia kuwa jibu mojawapo litakuwa “Marmaid.”

Ibada anayoikubali Mungu ni ibada ya unyenyekevu wa moyo, ibada ya utulivu, ibada ya kutaka kusikia neno la Mungu, ibada ya kuwaheshimu wanadamu wenzio, ibada ya kuuheshimu uhai aliouumba Mungu. Ibada ya kusherekea uumbaji wa Mungu katika siku ya sabato.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *