Makambi na Changamoto zake

Makambi katika kanisa kwa mda yalikuwa ni sherehe ya kutamanika, leo hii hali sivyo ilivyo tena. Makambi yamegeuka kuwa chukizo. Nina uhakika ya kuwa wale waumini walio na ari ya kujipumzisha kutokana na hali ngumu ya maisha wanayoipitia katika maisha yao hawapati pumziko lolote katika makambi na MUNGU PIA HAFURAHISHWI jinsi makambi yanavyoendeshwa.

Wanaoudhi sana ni wale Guest speakers ambao mlo ndio huwa wanausifu. Siku ya sabato jioni wanapomalizia makambi utawasikia wakiwasifia watu wa jikoni. Si vibaya… lakini ni vibaya. Sifa zimepelekea zinaa kuingia kwenye Kambi hata wewe msomaji ni shahidi.

Huwa inaudhi sana kanisa andalizi la kambi linapobagua diets za wageni na diets za wenyeji. Tafakari wakati wa Yesu, Wanafunzi wa Yesu ambao waliwahi msalimu na kuiona miujiza yake, wakati wa maankuli, hawakutengwa kuwa wa ‘HIGH TABLE.’ HIGH TABLE ni upumbavu na ni ibada ya kishenzi iliyoletwa katika NYUMBA YA MUNGU. Mtapokea kichapo! Badala ya kuhubiri kazi yenu kujaza matumbo kama Hophni na Phinehas na ku-brag kuhusu idadi ya makambi mtaenda as if nyinyi ndio cream ya Mungu!

Unadhani wakati wewe umeletewa mapochopocho katika meza vikiwemo mikate, mayai matunda na vyakula vingine vyororo yet yule utakayemhubiria amepewa kopo la uji na andazi moja, na anajua kuwa umeletewa si chuki tu ndiyo itakuwa moyoni mwake akikutazama? Ata-feel aje yet yeye ndiye alishurutishwa achangie chakula. Tafadhali, acheni kuongeza hatia kwa nyingine. Watu wote na wapewe chakula kilekile. Kama mhudumu ana shida fulani, hebu na awajulishe wasimamizi. Ikiwa hali yake ya unyonge itawapelekea wengine kutenda dhambi, hilo jukumu lake na alichukue mtu mwingine kwa sababu kanisani talanta nyingi hufinyiliwa chini ifikiapo mikutano ya hadhara ikiwemo makambi, wengi wakiwa na na nia ya kudona ili kushiba.

Ndugu mpendwa, ni mara ngapi minong’ono imesikika kuwa kuna mapendeleo katika uchaguzi wa wahudumu wa Camp wanaotumwa kwenda makambi mengine? Usijiletee laana bure. Tumbo lako litaridhika lakini kwa Mungu utajibu kwa sababu hukumjali Mungu. Ulifurahia ulipoenda tours nyingi, hata kama maombi yako mengi hayakuwa na mguso wowote kwani uliifanya kazi kwa maringo. Laana nyingi iko kwa wale wahusika wa mitambo haswa watafuta njia ambao wana zinaa sana kando na vijana na wazee wengine.

Kwa wale wasimamizi wa makambi ambao wameleta laana kwa kufanya au kusababishadhambi, wakati wa kutubu ndio huu. Pamoja sisi wote tumekosea na twahitaji huruma ya Mungu ili atusaidie huduma yetu isiwe ya laana. “Yesu Kristo, Tuoshe kwa Damu yako ili tufae machoni pako na machoni pa Mungu, Sisi wadhambi. Mtume Roho mtakatifu akae kwetu ili atufunze yatupasayo, atukumbushe utakatifu, atuonye tuone makosa yetu ili tukutegemee kila wakati. Haya twayaomba yakubaliwe na Mungu Baba kupitia kwa Yesu Kristo rafiki wetu, Amina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *