No.5: Na Tumwabudu Mfalme Mtukufu

Natumwabudu huyo Mfalme, Sifa za nguvu zake zivume; Ni ngao ni ngome Yeye milele, Ndizo sifa zake kale na kale.

Tazameni ulimwengu huu, Ulivyoumbwa ajabu kuu; Sasa umewekwa pahali pake, Hata utimize majira yake.

Kwa ulinzi wako kwetu Bwana, Twakushukuru U mwema sana; Hupewa chakula kila kiumbe, Kila kitu kina mahali pake.

Wanadamu tu wanyonge sana, Twakutumaini Wewe Bwana; Kamwe haupungui wako wema, Mkombozi wetu Rafiki mwema. u

No. 4: Jina la Yesu, Salamu

Jina la Yesu, salamu! Lisujudieni, Ninyi mbinguni hukumu, Na enzi mpeni. Ninyi mbinguni hukumu, Na enzi mpeni.

Enzi na apewe kwenu, watetea dini; Mkuzeni bwana wenu, Na enzi mpeni. Mkuzeni bwana wenu, Na enzi mpeni.

Enyi mbegu ya rehema nanyi msifuni;Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni.Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni. 

Wenye dhambi kumbukeni ya msalabani.wa furaha msifuni, Na enzi mpeni.Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni.

Kila mtu duniani msujudieni,ote-kote msifuni, Na enzi mpeni. Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni.

Sisi na wao pamoja tu mumo sifani. Milele sifa ni moja, ni ‘enzi mpeni’.ilele sifa ni moja, ni ‘enzi mpeni.’

No. 3: Mungu Atukuzwe

Mungu atukuzwe, kwa mambo makuu, Upendo wake ulitupa yesu, Aliyejitoa maisha yake, Tuwe nao uzima wa milele.

CHORUS

   Msifu, msifu dunia sikia;

   Msifu, msifu, watu wafurahi;

   Na uje kwa baba, kwa yesu mwana

   Ukamtukuze kwa mambo yote.

Wokovu kamili zawadi kwetu,

Ahadi ya mungu kwa ulimwengu;

Wanaomwamini na kuungama,

Mara moja wale husamehewa.

Alitufundisha mambo makuu, Alihakikisha wokovu wetu; Lakini zaidi ajabu kubwa,Yesu atakuja na tutamwona.

No. 2: Twamsifu Mungu

Twamsifu Mungu, Mwana wa upendo, Aliyetufia na kupaa juu.

CHORUS

  Aleluya! Usifiwe, aleluya! Amin;   Aleluya usifiwe, utubariki.

Twamsifu mungu, roho mtukufu, Akatufunulia mwokozi wetu

Twamsifu mwana, aliyetufia, Akatukomboa na kutuongoza.

Twamsifu mungu, wa neema yote,Aliyetwaa dhambi, akazifuta.

Tuamshe tena, tujaze na pendo.Moyoni uwashe moto wa roho.