No.1: Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu

Umtakatifu! Mungu Mwenyezi! Alfajiri sifa zako tutaimba; Umtakatifu, Bwana wa huruma, Mungu wa vyote hata milele.

Umtakatifu! Na malaika Wengi sana wanakuabudu wote; Elfu na maelfu wanakusujudu Wa zamani na hata milele.

U mtakatifu! Ingawa giza Lakuficha fahari tusiione, U mtakatifu! Wewe peke yako Kamili kwa uwezo na pendo.