Nyimbo

No. 130: Yesu Kwetu Ni Rafiki

Yesu kwetu ni rafiki, hwambiwa haja pia; Tukiomba kwa Babaye, maombi asikia; Lakini twajikosesha, twajitweka vibaya; Kama tulimwomba Mungu, dua alisikia.

Una dhiki na maonjo? una mashaka pia? Haifai kufa moyo, dua atasikia, Hakuna mwingine Mwema, wa kutuhurumia; Atujua tu dhaifu; maombi asikia.

Je, hunayo hata nguvu, huwezi kwendelea, Ujapodharauliwa, ujaporushwa pia, Watu wakikudharau, wapendao dunia, Hukwambata mikononi, dua atasikia.

Pata nyimbo Zaidi katika huu ukurasa ama Search